HUDUMA ZA MANA

Lengo kuu la Huduma hii ni kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa watu wote.

Fahamu zaidi...
 
 


    Vipindi vya Redio

Ili kulileta Neno la Mungu karibu na wewe zaidi, Huduma ya Mana inaandaa na kurusha baadhi ya mafundisho ya Neno la Mungu kwa njia ya redio kadhaa hapa nchini Tanzania.

Ili kufahamu zaidi redio hizo na siku na saa ya vipindi vyetu, bonyeza hapa.

   


BARUA YA MWEZI JULAI 2016

 Bwana Yesu asifiwe sana!

        Tunakuandikia barua hii tukiwa mjini Singida, ambapo leo tunaanza semina ya Siku tano.

Mwezi huu wa Julai tumeanza semina ya siku 8 mjini Mwanza. Tulikuwa tunajifunza somo linalohusu kujifunza jinsi Mungu anavyoongea na watu ili waweze kufuata vyema maelekezo yake. Semina hiyo ya Mwanza tuliifanya tarehe 3 10 Julai 2016.

         Na wiki iliyofuata yaani wiki iliyopita tarehe 14 17 Julai 2016 tulikuwa na semina nyingine mjini Shinyanga. Wakati wa semina hii tulijifunza aina za maombi yanayotengeneza mazingira ya Mungu kutusaidia.

         Na wiki hii tutakuwa hapa mjini Singida kwa siku 5 yaani leo tarehe 20 Julai hadi 24 Julai 2016.

         Ndani ya barua hii tunataka tukushirikishe hatua kadhaa za kufanya katika kuombea tatizo la kurithi, linalokwamisha mafanikio yako, ili lipate kuondoka maishani mwako.

                Hatua ya 1:

         Amua ni tatizo lipi la kurithi unalotaka Mungu akusaidie kuliondoa. Je, ni ugonjwa? Je, ni tabia? Je, ni hali ya maisha? Je, ni tatizo la Ki-imani? Je, ni tatizo la kushindwa kuoa au kuolewa?

                Hatua ya 2:

          Ikiwa hujui ikiwa tatizo linalokwamisha mafanikio yako ni la kurithi au sivyo mwombe Mungu akujulishe, na akupe maelekezo ya namna ya kuliombea ili liishe.

          Ukisoma yaliyotokea kipindi cha mfalme Daudi katika kitabu cha 2 Samweli 21:1, utaona ya kuwa wakati wa utawala wake, alipata tatizo la ukame kwa mfululizo wa miaka mitatu. Na alipomuuliza Mungu kwa njia ya maombi aliambiwa ya kuwa tatizo lile la ukame chanzo chake kilitokana na kosa alilofanya mfalme aliyemtangulia yaani mfalme Sauli. Na Mungu akampa maelekezo juu ya kipi kifanyike ili ule ukame uishe. Mfalme Daudi alitekeleza maelekezo aliyopewa na Mungu na tatizo la ukame likaisha.


                                                                          Endelea kusoma >>>  

 
Mitandao ya Kijamii
 
 
     

 

 

 

 

 

 

Ibariki Israeli Pamoja Nasi

Habari za Huduma

Mafundisho ya neno la Mungu

 
Sasa unaweza kutembelea taifa la Israeli kwa mafunzo ya kiroho pamoja nasi mara nne kwa mwaka. Kufahamu zaidi kuhusu huduma ya Israeli,
Bonyeza Hapa.
Karibu ufuatilie habari ,matukio na mabadiliko mbalimbali  yanayohusu huduma ya MANA pamoja na watendajikazi katika huduma.
Bonyeza Hapa kwa maelezo zaidi
Karibu ujisomee mafundisho ya Neno la Mungu katika tovuti hii sasa.
Bonyeza hapa
 
 
 
|Home|  |Kuhusu MANA |    |Nunua|      |Mafundisho|     |Maombi|     |Ratiba|   |Shuhuda|   |Barua Za Mwezi|   |Israel|

Haki zote zimehifadhiwa Huduma Ya MANA TANZANIA.