HUDUMA ZA MANA

Lengo kuu la Huduma hii ni kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa watu wote.

Fahamu zaidi...
 
 


    Vipindi vya Redio

Ili kulileta Neno la Mungu karibu na wewe zaidi, Huduma ya Mana inaandaa na kurusha baadhi ya mafundisho ya Neno la Mungu kwa njia ya redio kadhaa hapa nchini Tanzania.

Ili kufahamu zaidi redio hizo na siku na saa ya vipindi vyetu, bonyeza hapa.

   

IBARIKI ISRAEL PAMOJA NASI.

       Mwaka 2007 mwezi wa Desemba, tukiwa nchini Israel, Mungu alisema nasi juu ya kuwahimiza watu wake wajiunganishe na nchi ya Israel Kibiblia.
Na kwa kufanya hivyo watakuwa wanaibariki nchi ya Israel, kama sehemu ya maagizo ambayo Mungu amewapa watu wake ulimwengu mzima.
        Agizo hili lilikuwa ni sehemu ya hatua mojawapo muhimu katika kupanuka kwa huduma ambayo Mungu ametupa katika nchi ya Tanzania, na nchi nyingine ulimwenguni. Hii ndiyo sababu ya kukutaka uungane nasi katika kuibariki nchi ya Israeli. Tunajua ya kuwa hakuna mtu anayeibariki nchi ya Israeli, naye asibarikiwe na Mungu wa Ibrahimu, Isaka na wa Yakobo (Israeli).
        Mungu aliahidi jambo hili katika kitabu cha Mwanzo 12:3 alipomwambia Ibrahimu ya kuwa:”….Nitawabariki wakubarikio….Na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa”. Unaweza kuungana nasi katika kuibariki Israeli kwa njia zifuatazo:


      1.    OMBEA NCHI YA ISRAELI
Nchi ya Israeli haipo pale kama nchi kwa ajili ya raia wake tu, na kwa watu waishio ndani yake tu; lakini iko pale ili Mungu aitumie kwa ajili ya kujijulisha na kuwafikia watu wote ulimwenguni. Kumbuka ya kuwa Mungu anaitumia nchi ya Israel kama Lango la kupitisha yale yote aliyokusudia uyapate kutokana na agano lake alilolifanya na Ibrahimu. Unapoiombea Israeli – Mungu anailinda na kuitunza ili itumike kupitisha vitu ambavyo Mungu anataka vikufikie.
      2.    OMBEA MJI WA YERUSALEMU
Kufuatana na Ezekiel 26:2; “Yerusalemu” ni “lango la kabila za watu”. Tena kufuatana na Mathayo 5:35; “Yerusalemu” ni “mji wa mfalme mkuu” …yaani Yesu Kristo! Ikiwa umeungwa kwa Kristo Yesu, basi mji huu wa Yerusalemu unakuhusu sana! Ni lango la Mungu kwa ajili ya kabila za watu – na wewe ukiwa mmojawapo! Ndiyo maana katika Zaburi 122:6 tunahimizwa kuuombea mji huu amani na kuupenda!
       3.    UWE NA BENDERA YA ISRAELI
Jitahidi uwe na bendera kadhaa za nchi ya Israel. Halafu ziweke au zipeperushe ofisini kwako, au sehemu yako ya biashara, au nyumbani kwako, au mahali pengine panapokuhusu wewe binafsi kama vile Roho Mtakatifu atakavyokuongoza. Hii itakuwa nafasi ya kueleza uhusiano wako na taifa la Israeli kama uzao wa Ibrahimu kwa Imani uliyonayo katika Kristo Yesu. Hii ni sawa na mstari wa Wagalatia 3:29 usemao:”Na kama ninyi ni wa Kristo,basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi”

       4.    FUTA LAANA DHIDI YA NCHI YA ISRAELI ZILIZOTAMKWA KUTOKEA TANZANIA.
Mungu alimwambia Ibrahimu ya kuwa:”…Akulaaniye nitamlaani…” (Mwanzo 12:3) kumbuka ya kuwa kuwepo kwa taifa la Israeli ni tunda mojawapo la agano kati ya Mungu na Ibrahimu. Kwa hiyo unaposikia mtu yeyote ambaye ni mtanzania anailaani nchi ya Israeli; au si mtanzania lakini anailaani Israeli akiwa katika nchi ya Tanzania – usikae kimya! Unayo mamlaka katika jina la Yesu kutumia Damu ya Yesu (i) kuomba toba kwa ajili ya, na kwa niaba ya Tanzania kwa ajili ya laana hiyo dhidi ya nchi ya Israeli; (ii) kuomba maombi ya kuifuta laana hiyo, na badala yake achilia maneno ya kuibariki nchi ya Israeli.

 

Endelea  >>

 
Mitandao ya Kijamii
 
 
     

 

 

 

 

 

 

     
  Ibariki Israeli Pamoja Nasi Habari za Huduma Mafundisho ya neno la Mungu  
Sasa unaweza kutembelea taifa la Israeli kwa mafunzo ya kiroho pamoja nasi mara nne kwa mwaka. Kufahamu zaidi kuhusu huduma ya Israeli,
Bonyeza Hapa.
Karibu ufuatilie habari ,matukio na mabadiliko mbalimbali  yanayohusu huduma ya MANA pamoja na watendajikazi katika huduma.
Bonyeza Hapa kwa maelezo zaidi
Karibu ujisomee mafundisho ya Neno la Mungu katika tovuti hii sasa.
Bonyeza hapa
 
 
|Home|  |Kuhusu MANA|    |Nunua|      |Mafundisho|     |Maombi|     |Ratiba|   |Shuhuda|   |Barua Za Mwezi|   |Israel|

Haki zote zimehifadhiwa © Huduma Ya MANA TANZANIA.