HUDUMA ZA MANA

Lengo kuu la Huduma hii ni kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa watu wote.

Fahamu zaidi...
 
 


    Vipindi vya Redio

Ili kulileta Neno la Mungu karibu na wewe zaidi, Huduma ya Mana inaandaa na kurusha baadhi ya mafundisho ya Neno la Mungu kwa njia ya redio kadhaa hapa nchini Tanzania.

Ili kufahamu zaidi redio hizo na siku na saa ya vipindi vyetu, bonyeza hapa.

   

RIPOTI SEMINA YA SINGIDA (01 - 05 MEI 2013).

Utangulizi

         Tunamshukuru Mungu kwa kuifanikisha semina hii ya Singida, tunayo kila sababu ya kumshukuru Mungu sana kwa kutulinda toka tunaianza hadi tunamaliza semina hii. Pia katika semina hii Mungu alijidhihirisha kwa kiwango tofauti hivyo kuifanya semina hii kuwa ya kipekee kabisa.

         Semina hii ya Singida tuliifanya kuanzia tarehe 01 Mei hadi tarehe 05 meii 2013, ndani ya hema tuliyoisimamisha katika viwanja vya Peoples. Mahudhurio yalikuwa watu 5,000 hadi 6,000 au zaidi kwa siku. Pia  mahudhurio ya wasikilizaji kwa njia ya mtandao ilikuwa ni kati ya watu 3000 hadi 4000 kwa siku.

 Jumla ya watu 501 waliweza kuokoka katika semina hiyo.

Somo lililofundishwa

  Kichwa cha somo kilikuwa  “ SADAKA INAVYOUNGANISHA KIWANGO CHA UCHAJI NA UWEPO WA MUNGU”.

  Lengo la semina hii lilikuwa: Ni ili uweze kuongeza kiwango chako cha kumcha Mungu katika uwepo wa Mungu uliodhihirika kwako, na tunajifunza hili somo kwa njia ya utoaji wa sadaka.

 Pointi tano zilizoweka msingi wa somo.

  1. Maana ya kumcha Mungu – Ni hofu ya Mungu inayotokana na udhihirisho wa Mungu mahali hapo ambapo pametokea hofu ya Mungu. Mithali 8:13 “Kumcha Bwana ni kuchukia uovu”. Mithali 1:7,
  2. Utoaji sadaka ipasavyo ni njia mojawapo ya kufungulia uwepo wa Mungu udhihirike. 1Wafalme 18:36 – 39, Habakuki 2:14; Mungu alipoiumba dunia alitaka wanadamu wakae katika utukufu wa Mungu kama vile samaki anavyoishi ndani ya maji. Warumi 3:23,
  3. Mungu anatumia utoaji wa sadaka palipo na udhihirisho wake kumfundisha mtoaji juu ya kumcha Mungu. Kumbukumbu 14:22 – 23,
  4. Mungu anapima kiwango chako cha uchaji unapotoa sadaka yako mahali ambapo uwepo wake umedhihirika. Mwanzo 22:1 – 2, 12.
  5. Kiwango chako cha kumcha Mungu kinampa Mungu kiwango cha kukujibu maombi yako. Mwanzo 22:12, 15 – 18, Waebrania 5:7, Kuna kiwango cha maombi Mungu hawezi kukujibu mpaka amepima kiwango chako cha uchaji

  Endelea>>>

 
Mitandao ya Kijamii
 
 
     

 

 

 

 

 

 

     
 

Ibariki Israeli Pamoja Nasi

Habari za Huduma

Mafundisho ya neno la Mungu

 
Sasa unaweza kutembelea taifa la Israeli kwa mafunzo ya kiroho pamoja nasi mara nne kwa mwaka. Kufahamu zaidi kuhusu huduma ya Israeli,
Bonyeza Hapa.
Karibu ufuatilie habari ,matukio na mabadiliko mbalimbali  yanayohusu huduma ya MANA pamoja na watendajikazi katika huduma.
Bonyeza Hapa kwa maelezo zaidi
Karibu ujisomee mafundisho ya Neno la Mungu katika tovuti hii sasa.
Bonyeza hapa
 
 
|Home|  |Kuhusu MANA |    |Nunua|      |Mafundisho|     |Maombi|     |Ratiba|   |Shuhuda|   |Barua Za Mwezi|   |Israel|

Haki zote zimehifadhiwa © Huduma Ya MANA TANZANIA.