Mafundisho Archives - Mana http://mwakasege.org/category/mafundisho/ Mana Tue, 21 May 2024 10:07:48 +0000 en-US hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.7 https://i0.wp.com/mwakasege.org/wp-content/uploads/2022/03/cropped-Huduma-ya-Mana.png?fit=32%2C32&ssl=1 Mafundisho Archives - Mana http://mwakasege.org/category/mafundisho/ 32 32 203482993 SALAMU ZA PASAKA 2024 https://mwakasege.org/pasaka2022/?utm_source=rss&utm_medium=rss&utm_campaign=pasaka2022 Fri, 29 Mar 2024 12:04:36 +0000 http://beta.unitedthemes.com/brooklyn/?p=4104 Bwana Yesu asifiwe. Heri ya Pasaka ya 2024! Pamoja na salamu hizo, nataka kukujulisha msaada uliomo ndani ya ufufuo wa Yesu Kristo ili uyashinde majaribu. Lengo kubwa la majaribu, bila kujali chanzo chake, ni kuijaribu au kuipima “Imani” ya mtu (Yakobo 1:2,3). Ingawa mazingira yanayoweza kutafsiriwa na mtu ya kuwa ni jaribu kwake ni mengi, […]

The post SALAMU ZA PASAKA 2024 appeared first on Mana.

]]>

Bwana Yesu asifiwe.
Heri ya Pasaka ya 2024!

Pamoja na salamu hizo, nataka kukujulisha msaada uliomo ndani ya ufufuo wa Yesu Kristo ili uyashinde majaribu.
Lengo kubwa la majaribu, bila kujali chanzo chake, ni kuijaribu au kuipima “Imani” ya mtu (Yakobo 1:2,3).

Ingawa mazingira yanayoweza kutafsiriwa na mtu ya kuwa ni jaribu kwake ni mengi, lakini vyanzo vikuu vya majaribu ni hivi vifuatavyo:

Chanzo cha kwanza ni Shetani. Biblia inasema: “Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi” (Mathayo 4:1). Shetani anapomjaribu mtu, anatengeneza mazingira yatakayotumika kupima imani ya huyo mtu. Shetani anataka katika jaribu hilo, imani ishindwe kumsaidia huyo mtu kuvuka na kulishinda jaribu hilo, ili hatimaye aamue kuiacha imani aliyo nayo kwa Mungu katika Yesu Kristo.

Chanzo cha pili ni Mungu. Biblia inasema: “Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu…” (Mwanzo 22:1)
Mungu anapomjaribu mtu, huwa anatengeneza mazingira atakayotumia kupima uwezo wa imani aliyonayo, kama imefikia kiwango cha kuibeba hatua inayofuata ya majukumu na msaada aliompangia huyo mtu.

Jaribu kama hili, ni kama mtihani ambao mwanafunzi anapewa kupima uwezo alionao, ikiwa unaweza kubeba masomo ya darasa linalofuata. Ndiyo maana biblia inasema juu ya “toka imani hata imani” (Warumi 1:17). Hii inatupa kujua ya kuwa, kuna ngazi tofauti tofauti za imani, na uwezo wake unatofautiana.

Ndiyo maana mtu anapopokea anachopokea toka kwa Mungu, huwa anapokea kwa kadri ya kiwango cha imani alichonacho!
Chanzo cha tatu ni Tamaa. Biblia inasema: “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe…” (Yakobo 1:14).

Neno “tamaa”, kwa jinsi lilivyotumika kwenye mstari huu, lina maana ya msukumo ambao mtu anakuwa nao, unaomsukuma moyoni mwake, ili afanye mambo nje ya mapenzi ya Mungu.
Tamaa inapotumika kama chanzo cha jaribu kwa mtu, lengo lake ni kuipima imani ya mtu, kwa nia ya kuikwamisha ili mtu huyo asitoe ushirikiano kwa Roho Mtakatifu.

Ndiyo maana biblia inasema: “Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayoyataka” (Wagalatia 5:16,17).

Na hili lifuatalo unalijua? Ninalotaka ulijue kama hulijui ni kwamba, unapokutana na jaribu kubwa la imani yako, ni kiashiria kinachokujulisha ya kuwa, mbele yako kuna hatua muhimu ambayo Mungu anataka kukupa.

Jaribu toka kwa Shetani, linataka imani yako isikusaidie kulishinda, ili imani hiyo uiache. Na ukiiacha hiyo imani, na kesho yako aliyokupangia Mungu hutaipata (Waebrania 3:16 – 19).

Jaribu toka kwa Mungu, litakujengea msuli wa imani, ili iwe msingi mzuri wa kubebea kesho yako. Soma Yakobo 1:2 – 4
Jaribu toka kwenye Tamaa ya mwili, linatafuta katika mazingira yaliyopo, usiwe na uhakika moyoni mwako juu ya kipi cha kufanya, ili kuifikia kesho yako ambayo Mungu amekupangia (Wagalatia 5:16, 17 na Warumi 8:14).

Kwa mfano, Yesu alipokuwa anakaribia kuanza rasmi huduma yake, alikutana na jaribu kubwa toka kwa Shetani (Mathayo 4:1 – 11). Lakini Mungu akamsaidia kushinda! Na mlango ukafunguka wa kuanza huduma yake.

Tena, Yesu alikutana na jaribu kubwa muda mchache kabla ya kusalitiwa na kusulubishwa. Mwili ulikuwa ukishindana na roho yake, juu ya kuyafanya mapenzi ya Mungu ya kunywa kikombe, yaani msalaba (Mathayo 26:36 – 46). Lakini jaribu hili pia, Mungu alimsaidia kulishinda! Na mlango ukafunguka wa Yesu kusulubiwa na kufa na kufufuka!

Yesu alipofufuka ilikuwa ishara mojawapo yenye ujumbe kwa wanadamu ya kwamba, kwa msaada wa nguvu za ufufuo wa Yesu, tunaweza kushinda jaribu lolote linalopima na kuijaribu imani tuliyonayo kwa Mungu katika Yesu Kristo.

Ndiyo maana tunasoma hivi juu ya uhusiano wa ufufuo wa Yesu na imani tuliyonayo kwake: “Tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure” (1 Wakorintho 15:14). “Na kama Kristo hakufufuka, Imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu” (1 Wakorintho 15:17)
Maneno haya “imani yenu ni bure” yana maana ya kuwa imani yetu haina faida, kama Kristo hakufufuka. Hii inatupa kufahamu ya kuwa, kwa kuwa Kristo amefufuka, ina maana imani yetu si bure, bali imani yetu ina faida.

Na faida mojawapo tunayoipata katika Yesu aliyesulubiwa na aliyekufa na aliyefufuka, ni imani hiyo kutupa msaada wa kushinda majaribu tunayokutana nayo!
Kwa nini faida ya imani hii imeunganishwa na kufufuka kwa Yesu? Zipo sababu nyingi, lakini leo nikutajie hizi chache, ili zikupe moyo wa kumshukuru Mungu kwa kumfu
fua Yesu kutoka kwa wafu!

Sababu ya kwanza:

Yesu Kristo ndiye anadumu kutuombea. Na jambo mojawapo analotuombea, ni ili tupate msaada wa Mungu wa kuyashinda majaribu.

Biblia inasema: “Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea” (Warumi 8:34). Soma pia
Waebrania 7:22 – 25.
Yesu alimwombea Petro, na Petro akashinda jaribu lake. (Luka 22:31, 32). Na Yesu anakuombea na wewe, na utashinda jaribu lako!

Sababu ya Pili:

Yesu alipofufuka ilikuwa pia ni ishara ya kutujulisha ya kuwa, malipo ya dhambi zetu aliyoyafanya Yesu pale msalabani, yamekubaliwa na Mungu.
Ndiyo maana imeandikwa ya kuwa: “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu, kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti” (Warumi 8:1, 2).

Jambo hili lilifanya shetani na tamaa za mwili, kupoteza uhalali wa kuendelea kutumia dhambi iliyotubiwa, kuishinda imani tuliyonayo katika Kristo Yesu.

Sababu ya tatu:

Nguvu za ufufuo zinaingia ndani yako unapompokea Kristo Yesu moyoni mwako, na kuokoka! Na kwa ajili hiyo, zinamfanya Mungu katika Yesu Kristo, awe pamoja na wewe, ili hata katika majaribu, bado upate nguvu na nia ya kuendelea kuyafanya mapenzi ya Mungu, bila kukata tamaa!
Biblia inasema: “Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa Kondoo, awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo” (Waebrania 13:20, 21).

Na ndiyo maana nguvu za ufufuo wa Yesu ndani yetu (Waefeso 1:17 – 23), zinatupa kushinda, “na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda” (Warumi 8:37).

Mimi na mke wangu, na watoto wetu, na timu nzima ya huduma yetu ya Mana, tunakutakia siku njema ya kukumbuka kufufuka kwa Yesu.

Tuzidi kuombeana. Tunakutakia pasaka njema!

The post SALAMU ZA PASAKA 2024 appeared first on Mana.

]]>
4104
Faida ya 3 ya kuombea akili za mtu. https://mwakasege.org/faida-ya-3-ya-kuombea-akili-za-mtu/?utm_source=rss&utm_medium=rss&utm_campaign=faida-ya-3-ya-kuombea-akili-za-mtu Sat, 28 May 2022 16:09:12 +0000 http://mwakasege.org/?p=5208 Leo tuangalie faida ya 3 ya kuombea akili za mtu. Faida hiyo ya 3 ni: “Mungu azisaidie akili zako, ziwe na hali ambayo hatazikataa bali atazikubali”. Mungu anasema hivi: “Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, na akili zao wenye akili nitazikataa” (1 Wakorintho 1:19). Mungu anapozikataa “akili zao wenye akili”, ina maana hatashirikiana nazo katika utendaji […]

The post Faida ya 3 ya kuombea akili za mtu. appeared first on Mana.

]]>
Leo tuangalie faida ya 3 ya kuombea akili za mtu. Faida hiyo ya 3 ni:
“Mungu azisaidie akili zako, ziwe na hali ambayo hatazikataa bali atazikubali”.
Mungu anasema hivi: “Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, na akili zao wenye akili nitazikataa” (1 Wakorintho 1:19).
Mungu anapozikataa “akili zao wenye akili”, ina maana hatashirikiana nazo katika utendaji wake! Mtu mwenye akili hizo, anaweza kuendelea kuzitumia akili hizo, lakini ya kwamba, atafanya akifanyacho, bila Mungu kuhusika na afanyacho, na bila Mungu kuwa upande wake, kwenye hicho afanyacho!
Zipo sababu kadhaa, zinazoweza kumfanya Mungu, azikatae “akili zao wenye akili”. Lakini kufuatana na mstari tuliosoma hapa juu, tunaona kuwa, aina ya hekima, inayotoka ndani ya akili, ina uhusiano mkubwa na Mungu kuzikataa akili.
Tukilitazama jambo hili kwa mtazamo huu, tutaona sababu kadhaa zifuatazo, zinazomfanya Mungu azikatae “akili zao wenye akili”!
Sababu ya 1:
Mungu anazikataa akili zao wenye akili, kwa sababu zinafanya kazi na hekima isiyo yake! Kufuatana na Ufunuo wa Yohana 17:9, akili zinatakiwa zifanye kazi na hekima ya Mungu. Hii ni kwa kuwa, akili ziliumbwa na Mungu (Ayubu 32:8), na kwa ajili hiyo, hekima inayotumika, ni lazima iwe ya Mungu.
Akili ikitumia hekima isiyo ya Mungu, Mungu anaiharibu hekima hiyo, na kuzikataa akili husika!
Sababu ya 2:
Mungu anazikataa akili zao wenye akili, kwa sababu akili zinatumia “hekima” ambayo imeuzarau msalaba wa Yesu na kuuona ni “upuuzi” (1 Wakorintho 1:22, 23).
Akili haifanyi sawa kushirikiana na hekima, inayodharau na kupuuzia msalaba wa Yesu, wakati biblia inasema msalaba huo ni “nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu” (1 Wakorintho 1:24).
Akili inapotumia hekima ya namna hii – kama ya Wayunani, Mungu anaiharibu hekima hiyo, na kuzikataa akili zao wenye akili, zilizobeba na kutumia hekima hiyo.
Sababu ya 3:
Mungu anazikataa akili zao wenye akili, kwa sababu hazimpi Yesu nafasi anayostahili, kama msingi wa maisha ya kila siku ya mtu, na msingi wa kazi za kila siku za mtu.
Biblia inatujulisha ya kuwa, Mungu aliiweka misingi ya nchi kwa kutumia hekima yake (Mithali 3:19). Na kwa ajili hiyo, akili za mtu zinatakiwa zimpe Yesu, nafasi ya kuwa msingi wa kila eneo la maisha ya mtu. Hii ni kwa kuwa, msalaba umemfanya Yesu awe “kwetu hekima itokayo kwa Mungu” (1 Wakorintho 1:30). Na kwa sababu hiyo, chochote ukifanyacho bila kutumia hekima ya Yesu, hakitakuwa na msingi imara.
Sababu ya 4:
Mungu anazikataa akili zao wenye akili, pale zisipotoa nafasi, kwa hekima ya Mungu itumike kumsaidia mtu: Kujua wakati wa kuongea; kujua namna ya kuongea; na kujua wakati wa kunyamaza kimya.
Biblia inasema: Mungu anawapa watu wake, “Kinywa na hekima” (Luka 21:14), ili wajue cha kusema, na wakati wa kusema, na namna ya kusema.
Lakini pia, biblia inatujulisha ya kuwa, kuna “kunyamaza” ambako ni matokeo, ya hekima ndani ya mtu, inayomsukuma anyamaze asiongee!
Imeandikwa hivi: “Laiti mngenyamaza kabisa! Hilo lingekuwa hekima kwenu” (Ayubu 13:5).
Kumbuka: Unapoombea Mungu azisaidie akili zako, ziwe na hali ambayo hatazikataa, bali atazikubali, usisahau kuomba toba kwake, ikiwa mojawapo ya sababu hizo nne, inakuhusu, au zote zinakuhusu.
Hii itampa Mungu nafasi ya kukusamehe, na kujibu maombi haya juu ya akili zako!

The post Faida ya 3 ya kuombea akili za mtu. appeared first on Mana.

]]>
5208
Faida za kuombea akili, ili kuimarisha Imani yako, maisha yako-2 https://mwakasege.org/faida-za-kuombea-akili-ili-kuimarisha-imani-yako-maisha-yako-2/?utm_source=rss&utm_medium=rss&utm_campaign=faida-za-kuombea-akili-ili-kuimarisha-imani-yako-maisha-yako-2 Thu, 12 May 2022 15:37:22 +0000 http://mwakasege.org/?p=5177 Bwana Yesu asifiwe tena na tena…hata milele! Leo, nataka nikuletee faida ya 2, inayotokana na mtu, kuombea akili zake. Hii ni sehemu ya mfululizo wa somo, tuliloanza kusoma tarehe 05/05/2022. Somo hilo lina kichwa kinachosema hivi: “Faida za kuombea akili, ili kuimarisha Imani yako, maisha yako”. Faida ya 2 ya kuombea akili ni: “Kuziwezesha akili […]

The post Faida za kuombea akili, ili kuimarisha Imani yako, maisha yako-2 appeared first on Mana.

]]>
Bwana Yesu asifiwe tena na tena…hata milele!
Leo, nataka nikuletee faida ya 2, inayotokana na mtu, kuombea akili zake. Hii ni sehemu ya mfululizo wa somo, tuliloanza kusoma tarehe 05/05/2022. Somo hilo lina kichwa kinachosema hivi: “Faida za kuombea akili, ili kuimarisha Imani yako, maisha yako”.
Faida ya 2 ya kuombea akili ni: “Kuziwezesha akili zako, zikubali kufanya kazi, chini ya uongozi wa amani ya Kristo”.
Biblia inasema katika Wafilipi 4:6, 7 ya kuwa: “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu”.
“Akili zote” katika mstari huu ina maana fikra zote, na mawazo yote, na mitazamo yote, na uelewa wote, na ufahamu wote unaotokana na akili!
Hebu tuitizame kwa pamoja faida hii, kwa kuangalia mfano wa eneo lifuatalo:
“Kutafuta uongozi wa Mungu, juu ya jambo lolote”.
Mithali 23:4b inasema: “…acha kuzitegemea akili zako mwenyewe”. Na Mithali 3:5 inasema: “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe”.
Ingawa Biblia inaturuhusu, na kutuhimiza kuzitumia akili (Waebrania 5:14), lakini inatukataza tusizitegemee akili. Biblia inatuhimiza tuitumie “amani ya Mungu”, kuthibiti matumizi ya “akili zote” (Wafilipi 4:7).
Na kwa sababu hiyo, hutakiwi kuzitegemea akili (au fikra au mawazo), katika kutafuta uongozi wa Mungu, juu ya jambo lolote, bali tegemea amani ya Kristo, katika kuchagua ni fikra ipi ya kuifuata, au ni wazo lipi la kulifuata.
Hii ni kwa sababu, fikra na mawazo katika akili zako, si za kutegemewa kukuongoza, bila amani ya Mungu kuhusika!
Biblia inasema: Katika kila wazo, au fikra, au neno…“Utafute amani ukaifuate” (Zaburi 34:14). Na kwa sababu hiyo – “mtaongozwa na amani” (Isaya 55:12b).
Na ikiwa fikra, au wazo, vinakuongoza kwenye njia iliyopotoka, nje ya Mungu, utajikuta umekosa amani moyoni mwako!
Hii ni kwa sababu, wale wapitao katika njia iliyopotoka, hawana amani mioyoni mwao (Isaya 59:8). Tena “Wala njia ya amani hawakuijua” (Warumi 3:17).
Angalizo: Fikra yo yote moyoni mwako, isiyokubali kutawaliwa na kuongozwa na amani ya Kristo, usiifuate! Na usilifuate wazo lolote moyoni mwako, lisilokubali kutawaliwa, na kuongozwa na amani ya Kristo!
Kumbuka:
Jizoeze kuombea akili zako, na fikra zako, na mawazo yako, na mtazamo wako, vikubali kutawaliwa, na kufanya kazi chini ya amani ya Mungu, iliyo moyoni mwako kwa njia ya Yesu Kristo. Akili zako unapozitumia, zisipotoa ushirikiano kwa amani ya Mungu ndani yako, ni rahisi zikakupotosha na wakati huo huo usijue kama umepotoka!

The post Faida za kuombea akili, ili kuimarisha Imani yako, maisha yako-2 appeared first on Mana.

]]>
5177
Faida za kuombea akili, ili kuimarisha imani yako, na maisha yako-1 https://mwakasege.org/kuombea-akili/?utm_source=rss&utm_medium=rss&utm_campaign=kuombea-akili Thu, 05 May 2022 16:01:20 +0000 http://beta.unitedthemes.com/brooklyn/?p=4098 Bwana Yesu asifiwe Tunaamini unaendelea vizuri. Leo nataka nianze kukuletea mfululizo wa masomo, yanayohusu: “Faida za kuombea akili, ili kuimarisha imani yako, na maisha yako”. Ninapoziandika faida hizi, siziandiki kwa mtiririko wa umuhimu. Naziandika kwa mtiririko wa mfuatano wa kiuandishi tu, faida zote ni muhimu! Faida ya 1 ya kuombea akili: MUNGU AKUSAIDIE, KUJUA MATUMIZI […]

The post Faida za kuombea akili, ili kuimarisha imani yako, na maisha yako-1 appeared first on Mana.

]]>
Bwana Yesu asifiwe
Tunaamini unaendelea vizuri. Leo nataka nianze kukuletea mfululizo wa masomo, yanayohusu: “Faida za kuombea akili, ili kuimarisha imani yako, na maisha yako”. Ninapoziandika faida hizi, siziandiki kwa mtiririko wa umuhimu. Naziandika kwa mtiririko wa mfuatano wa kiuandishi tu, faida zote ni muhimu!

Faida ya 1 ya kuombea akili:

MUNGU AKUSAIDIE, KUJUA MATUMIZI YA AKILI ALIZOKUPA, ILI UWEZE KUZITUMIA IPASAVYO, KAMA ALIVYOKUSUDIA.
Mungu alipomuumba mtu, alimuumba awe jumlisho la roho, na nafsi, na mwili (2 Wakorintho 7:1). Mtu ni roho, anayo nafsi, na anakaa ndani ya mwili!
Mtu aliumbwa aweze kuishi, kwenye ulimwengu mbili kwa wakati mmoja – yaani ulimwengu wa kiroho, na ulimwengu wa kimwili kwa pamoja, na kwa wakati mmoja.
Mtu aliumbwa awe roho, ili kwa njia ya roho, aweze kuishi katika ulimwengu wa roho (Mwanzo 1:26, 27). Na kwa mwili wake, aweze kuishi katika ulimwengu wa kimwili (Mwanzo 2:7).
Na mtu alipewa nafsi, ili iwe “kiungo”, kati ya roho na mwili. Na kwa ajili ya jukumu hilo, nafsi ni kiungo muhimu cha mtu, katika kuunganisha maisha yake ya kiroho, na ya kimwili.
Ndiyo maana roho ya mtu, ndiyo iliyoumbwa kwanza (Mwanzo 1:27). Mwili wa mtu, uliumbwa wa pili (Mwanzo 2:7a). Na nafsi ya iliumbwa ya tatu (Mwanzo 2:7b)
Biblia inasema: “Bwana Mungu…, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai” (Mwanzo 2:7). Na ukisoma Ayubu 32:8; utasoma maneno haya: “Lakini imo roho ndani ya mwanadamu, na pumzi za Mwenyezi huwapa akili”.
Mistari hiyo miwili, inatupa kujua, na kuamini kuwa, akili imo ndani ya Nafsi!
Lakini pia, ni vizuri ujue ya kuwa, akili siyo ubongo, na ubongo siyo akili; ingawa vyote viwili viliumbwa ili vifanye kazi kwa kushirikiana! Ubongo umo katika mwili, na akili imo katika nafsi!
Biblia inatuelekeza tusizitegemee akili! Imeandikwa katika Mithali 3:5, 6; kuwa: “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako”.
Na Mithali 23:4 inasema: “…acha kuzitegemea akili zako mwenyewe”.
Pamoja na maagizo ya biblia, kwamba tusizitegemee akili, inatuhimiza pia, kuwa tuzitumie akili! Hii inatujulisha kuwa, Mungu aliziumba akili ndani ya kila mtu, ili azitumie, lakini asizitegemee!
Biblia inasema: “…Kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya” (Waebrania 5:13, 14).
Faida mojawapo ya kuombea akili, ni ili Mungu akusaidie kujua matumizi ya akili alizokupa, ili uweze kuzitumia hizo akili, kama alivyokusudia!
Tena, kumbuka, bila msaada wa Mungu, si rahisi sana ukaweza kuzitumia akili bila kuzitegemea! Lakini Mungu, anao uwezo wa kukusaidia, uweze kuzitumia akili, na usizitegemee, bali umtegemee Yeye!
Ombea akili ili ujue matumizi yake! Kitu usichojua matumizi yake, ni rahisi kukitumia vibaya; au hutakitumia kwa kiwango kinachotakiwa! Na kitu ulichonacho, na huijui faida yake kwako, si rahisi pia kukikumbuka kukiombea ipasavyo! Zijue faida za akili, ili uweze kukumbuka kuziombea mara kwa mara!
Tuzidi kuombeana katika hili!

The post Faida za kuombea akili, ili kuimarisha imani yako, na maisha yako-1 appeared first on Mana.

]]>
4098