Mana https://mwakasege.org/ Mana Thu, 18 Apr 2024 05:24:07 +0000 en-US hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.5.2 https://i0.wp.com/mwakasege.org/wp-content/uploads/2022/03/cropped-Huduma-ya-Mana.png?fit=32%2C32&ssl=1 Mana https://mwakasege.org/ 32 32 203482993 >>> Semina ya Neno la Mungu itafanyika Viwanja vya Wajenzi, Dodoma. Tarehe 17 Mpaka 21 April 2024 >>> https://mwakasege.org/tazama-semina-ya-mbeya-kuanzia-26-mpaka-30-oktoba-2022/?utm_source=rss&utm_medium=rss&utm_campaign=tazama-semina-ya-mbeya-kuanzia-26-mpaka-30-oktoba-2022 Wed, 03 Apr 2024 16:54:08 +0000 https://mwakasege.org/?p=5509 Bonyeza hapa kutazama sasa.

The post >>> Semina ya Neno la Mungu itafanyika Viwanja vya Wajenzi, Dodoma. Tarehe 17 Mpaka 21 April 2024 >>> appeared first on Mana.

]]>
Bonyeza hapa kutazama sasa.

The post >>> Semina ya Neno la Mungu itafanyika Viwanja vya Wajenzi, Dodoma. Tarehe 17 Mpaka 21 April 2024 >>> appeared first on Mana.

]]>
5509
SALAMU ZA PASAKA 2024 https://mwakasege.org/pasaka2024/?utm_source=rss&utm_medium=rss&utm_campaign=pasaka2024 Fri, 29 Mar 2024 16:00:36 +0000 http://beta.unitedthemes.com/brooklyn/?p=4104 Bwana Yesu asifiwe! Maneno ambayo Yesu aliyasema akiwa katika bustani ya Gethsemane masaa machache kabla Yuda hajamsaliti, yanatupa msukumo mkubwa wa kutaka kujifunza zaidi juu ya kuombea majaribu. Yesu alisema hivi: “Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu” (Mathayo 26:41). Leo nataka tujifunze umuhimu wa “Kumwomba Mungu akupe kujua chanzo […]

The post SALAMU ZA PASAKA 2024 appeared first on Mana.

]]>
Bwana Yesu asifiwe!
Maneno ambayo Yesu aliyasema akiwa katika bustani ya Gethsemane masaa machache kabla Yuda hajamsaliti, yanatupa msukumo mkubwa wa kutaka kujifunza zaidi juu ya kuombea majaribu.

Yesu alisema hivi: “Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu” (Mathayo 26:41).

Leo nataka tujifunze umuhimu wa “Kumwomba Mungu akupe kujua chanzo cha jaribu linalokukabili, na akupe msaada wa kulishinda”.
Hili ni muhimu kulijua kwa sababu, kujua chanzo cha jaribu, kunakupa na kunakuwezesha, uwe na msingi mzuri wa namna ya kulishinda jaribu husika.

Ni muhimu sana kukijua chanzo cha jaribu linalokuhusu. Hii ni kwa sababu, ingawa yapo majaribu ya aina “mbalimbali” (Yakobo 1:2), lakini majaribu hayo yanalenga kukijaribu kitu kimoja nacho ni “Imani” (Yakobo 1:3) ya yule anayejaribiwa!

Ukisoma na ukitafakari juu ya vyanzo vya majaribu kibiblia, utaona ya kwamba, ukikijua chanzo cha jaribu, utajikuta unajifunza kulitazama na kuliombea jaribu husika, kutoka kwenye nia ya lengo la anayekujaribu, kukuletea jaribu linalolenga imani yako.
Hebu tujifunze zaidi kwa kuangalia vyanzo vifuatavyo vya majaribu:

Mfano wa 1:
Chanzo cha jaribu kinapokuwa ni shetani.
Tunasoma katika Mathayo 4:1 ya kwamba: “Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na ibilisi”. Maneno ya mstari huu, yanatupa kufahamu ya kuwa chanzo kimojawapo ni Ibilisi au Shetani.
Lengo kubwa la Shetani kuijaribu imani ya mtu aliyonayo ndani ya Yesu Kristo, ni ili imani hiyo ishindwe kumsaidia katika jaribu hilo, hatimaye apate sababu ya “kujitenga na imani” hiyo (1 Timotheo 4:1).

Lakini, hata kama hatajitenga na imani, basi imani aliyonayo katika Yesu Kristo, iendelee kupungua nguvu, na ikibidi imani itindike au iishe kabisa (Luka 22:31, 32).

Biblia inasema, “Imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17). Hii ina maana ya kuwa jaribu la shetani kwenye imani yako, linalenga kukufanya upoteze tumaini lako kwenye uwezo wa Mungu kutimiza ahadi zake.

Tukisoma habari za kujaribiwa kwa Yesu na shetani, katika Mathayo 4:1 – 11 na katika Luka 4:1 – 13, tunajifunza mambo yafuatayo juu ya kushughulika na majaribu ambayo chanzo chake ni shetani:

Jambo la 1: Yesu aliweka nia ya kumshinda shetani kama mjaribu, katika lengo alilokuwa nalo (shetani), la kutaka Yesu aache kumtegemea Mungu na neno lake.
Ndiyo maana katika majaribu yote matatu ya Shetani, Yesu alimjibu Shetani kwa kusema “imeandikwa” (Mathayo 4:4, 7), ili Shetani ajue ya kuwa hata katikati ya majaribu, ataendelea kumtegemea Mungu na kulitumainia neno lake
Na wewe fanya vivyo hivyo unapokuwa katika jaribu, kama vile Yesu alivyofanya. Tafakari na kukiri mistari ya neno la Mungu, inayoahidi Mungu kukupa ushindi katika jaribu hilo. Na Mungu ataliangalia neno lake hilo, na kukutimizia (Yeremia 1:12).

Jambo la 2: Shetani alimsemesha Yesu, kwa namna ambayo, alitaka amuone Mungu siyo mwaminifu. Lakini Yesu alikataa wazo hilo la shetani kwa njia ya neno la Mungu na kwa maombi.

Na wewe unapoona jaribu linakuletea mawazo ya kuona kuwa, kumtegemea Mungu na neno lake hakujakusaidia kushinda jaribu hilo, na kwa ajili hiyo unajikuta unapoteza nia ya kuendelea na jambo ulilokuwa unalifanya, ujue nyuma ya jaribu hilo kuna Shetani!

Na inawezekana kwako wewe, imani yako ikawa bado ina nguvu hata kama ni kidogo; lakini wakati huo huo imani za wanaokuzunguka, nguvu za imani zao zimeisha. Na watu kama hao, utakuta wanazungumza na wewe maneno yanayokutaka uache kumtegemea Mungu wako, kwa kuwa wanaona ameshindwa kukusaidia.

Unakumbuka alichosema mke wa Ayubu kwa Ayubu baada ya imani yake kuishiwa nguvu, walipokuwa wamesongwa na majaribu?

Biblia inasema mke wa Ayubu alimwambia mume wake hivi: “Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu, ukafe. Lakini yeye (Ayubu) akamwambia, wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu wanenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake” (Ayubu 2:9, 10).

Hali hii iliwahi kumpata Daudi, kama tunavyosoma katika Zaburi 42:1 – 4. Je, kuna jaribu unalolipitia na unasikia kukata tamaa? Usikate tamaa na endelea kumwomba Mungu juu hali unayoipitia, naye atakusaidia (Luka 18:1).

Jambo la 3: Neno alilokuwa analitumia Yesu, alipokuwa anajaribiwa na Shetani, lililenga kuua nguvu za Shetani kwanza, ili kulifanya jaribu lipoteze nguvu za kumjaribu Yesu.

Na ndio maana kabla ya Yesu kumwambia Shetani kwa mara ya tatu kuwa “imeandikwa”; Yesu alimkemea kwanza Shetani ili aondoke.
Biblia inasema: “Ndipo Yesu alipomwambia, nenda zako shetani. Kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake, kisha Ibilisi akamwacha…” (Mathayo 4:10, 11).

Na tunaona pia ya kuwa Shetani alipokemewa na kuondoka, na majaribu pia yalikoma katika kipindi kile! Na wewe fanya vivyo hivyo! Ukijua ya kuwa ni shetani aliye chanzo cha jaribu lako, tumia neno la Mungu la biblia kumpinga, halafu mkemee na kumwamuru aondoke. Uwe na uhakika ataondoka!

Naamini umepata jambo la kukusaidia katika somo hili la leo.

Tunakutakia wiki njema ya sikukuu ya Pasaka.

 

The post SALAMU ZA PASAKA 2024 appeared first on Mana.

]]>
4104
Faida ya 3 ya kuombea akili za mtu. https://mwakasege.org/faida-ya-3-ya-kuombea-akili-za-mtu/?utm_source=rss&utm_medium=rss&utm_campaign=faida-ya-3-ya-kuombea-akili-za-mtu Sat, 28 May 2022 16:09:12 +0000 http://mwakasege.org/?p=5208 Leo tuangalie faida ya 3 ya kuombea akili za mtu. Faida hiyo ya 3 ni: “Mungu azisaidie akili zako, ziwe na hali ambayo hatazikataa bali atazikubali”. Mungu anasema hivi: “Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, na akili zao wenye akili nitazikataa” (1 Wakorintho 1:19). Mungu anapozikataa “akili zao wenye akili”, ina maana hatashirikiana nazo katika utendaji […]

The post Faida ya 3 ya kuombea akili za mtu. appeared first on Mana.

]]>
Leo tuangalie faida ya 3 ya kuombea akili za mtu. Faida hiyo ya 3 ni:
“Mungu azisaidie akili zako, ziwe na hali ambayo hatazikataa bali atazikubali”.
Mungu anasema hivi: “Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, na akili zao wenye akili nitazikataa” (1 Wakorintho 1:19).
Mungu anapozikataa “akili zao wenye akili”, ina maana hatashirikiana nazo katika utendaji wake! Mtu mwenye akili hizo, anaweza kuendelea kuzitumia akili hizo, lakini ya kwamba, atafanya akifanyacho, bila Mungu kuhusika na afanyacho, na bila Mungu kuwa upande wake, kwenye hicho afanyacho!
Zipo sababu kadhaa, zinazoweza kumfanya Mungu, azikatae “akili zao wenye akili”. Lakini kufuatana na mstari tuliosoma hapa juu, tunaona kuwa, aina ya hekima, inayotoka ndani ya akili, ina uhusiano mkubwa na Mungu kuzikataa akili.
Tukilitazama jambo hili kwa mtazamo huu, tutaona sababu kadhaa zifuatazo, zinazomfanya Mungu azikatae “akili zao wenye akili”!
Sababu ya 1:
Mungu anazikataa akili zao wenye akili, kwa sababu zinafanya kazi na hekima isiyo yake! Kufuatana na Ufunuo wa Yohana 17:9, akili zinatakiwa zifanye kazi na hekima ya Mungu. Hii ni kwa kuwa, akili ziliumbwa na Mungu (Ayubu 32:8), na kwa ajili hiyo, hekima inayotumika, ni lazima iwe ya Mungu.
Akili ikitumia hekima isiyo ya Mungu, Mungu anaiharibu hekima hiyo, na kuzikataa akili husika!
Sababu ya 2:
Mungu anazikataa akili zao wenye akili, kwa sababu akili zinatumia “hekima” ambayo imeuzarau msalaba wa Yesu na kuuona ni “upuuzi” (1 Wakorintho 1:22, 23).
Akili haifanyi sawa kushirikiana na hekima, inayodharau na kupuuzia msalaba wa Yesu, wakati biblia inasema msalaba huo ni “nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu” (1 Wakorintho 1:24).
Akili inapotumia hekima ya namna hii – kama ya Wayunani, Mungu anaiharibu hekima hiyo, na kuzikataa akili zao wenye akili, zilizobeba na kutumia hekima hiyo.
Sababu ya 3:
Mungu anazikataa akili zao wenye akili, kwa sababu hazimpi Yesu nafasi anayostahili, kama msingi wa maisha ya kila siku ya mtu, na msingi wa kazi za kila siku za mtu.
Biblia inatujulisha ya kuwa, Mungu aliiweka misingi ya nchi kwa kutumia hekima yake (Mithali 3:19). Na kwa ajili hiyo, akili za mtu zinatakiwa zimpe Yesu, nafasi ya kuwa msingi wa kila eneo la maisha ya mtu. Hii ni kwa kuwa, msalaba umemfanya Yesu awe “kwetu hekima itokayo kwa Mungu” (1 Wakorintho 1:30). Na kwa sababu hiyo, chochote ukifanyacho bila kutumia hekima ya Yesu, hakitakuwa na msingi imara.
Sababu ya 4:
Mungu anazikataa akili zao wenye akili, pale zisipotoa nafasi, kwa hekima ya Mungu itumike kumsaidia mtu: Kujua wakati wa kuongea; kujua namna ya kuongea; na kujua wakati wa kunyamaza kimya.
Biblia inasema: Mungu anawapa watu wake, “Kinywa na hekima” (Luka 21:14), ili wajue cha kusema, na wakati wa kusema, na namna ya kusema.
Lakini pia, biblia inatujulisha ya kuwa, kuna “kunyamaza” ambako ni matokeo, ya hekima ndani ya mtu, inayomsukuma anyamaze asiongee!
Imeandikwa hivi: “Laiti mngenyamaza kabisa! Hilo lingekuwa hekima kwenu” (Ayubu 13:5).
Kumbuka: Unapoombea Mungu azisaidie akili zako, ziwe na hali ambayo hatazikataa, bali atazikubali, usisahau kuomba toba kwake, ikiwa mojawapo ya sababu hizo nne, inakuhusu, au zote zinakuhusu.
Hii itampa Mungu nafasi ya kukusamehe, na kujibu maombi haya juu ya akili zako!

The post Faida ya 3 ya kuombea akili za mtu. appeared first on Mana.

]]>
5208
KIBIBLIA TUMBO LA UZAZI LA MWANAMKE NI NINI? https://mwakasege.org/kibiblia-tumbo-la-uzazi-la-mwanamke-ni-nini/?utm_source=rss&utm_medium=rss&utm_campaign=kibiblia-tumbo-la-uzazi-la-mwanamke-ni-nini Tue, 17 May 2022 15:52:47 +0000 http://mwakasege.org/?p=5180 Maombi Haya ni Matokeo ya Kongamano la Wanawake Waombaji lililofanyika arusha tar 3 Mei 2022.

The post KIBIBLIA TUMBO LA UZAZI LA MWANAMKE NI NINI? appeared first on Mana.

]]>
Maombi Haya ni Matokeo ya Kongamano la Wanawake Waombaji lililofanyika arusha tar 3 Mei 2022.

The post KIBIBLIA TUMBO LA UZAZI LA MWANAMKE NI NINI? appeared first on Mana.

]]>
5180
Faida za kuombea akili, ili kuimarisha Imani yako, maisha yako-2 https://mwakasege.org/faida-za-kuombea-akili-ili-kuimarisha-imani-yako-maisha-yako-2/?utm_source=rss&utm_medium=rss&utm_campaign=faida-za-kuombea-akili-ili-kuimarisha-imani-yako-maisha-yako-2 Thu, 12 May 2022 15:37:22 +0000 http://mwakasege.org/?p=5177 Bwana Yesu asifiwe tena na tena…hata milele! Leo, nataka nikuletee faida ya 2, inayotokana na mtu, kuombea akili zake. Hii ni sehemu ya mfululizo wa somo, tuliloanza kusoma tarehe 05/05/2022. Somo hilo lina kichwa kinachosema hivi: “Faida za kuombea akili, ili kuimarisha Imani yako, maisha yako”. Faida ya 2 ya kuombea akili ni: “Kuziwezesha akili […]

The post Faida za kuombea akili, ili kuimarisha Imani yako, maisha yako-2 appeared first on Mana.

]]>
Bwana Yesu asifiwe tena na tena…hata milele!
Leo, nataka nikuletee faida ya 2, inayotokana na mtu, kuombea akili zake. Hii ni sehemu ya mfululizo wa somo, tuliloanza kusoma tarehe 05/05/2022. Somo hilo lina kichwa kinachosema hivi: “Faida za kuombea akili, ili kuimarisha Imani yako, maisha yako”.
Faida ya 2 ya kuombea akili ni: “Kuziwezesha akili zako, zikubali kufanya kazi, chini ya uongozi wa amani ya Kristo”.
Biblia inasema katika Wafilipi 4:6, 7 ya kuwa: “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu”.
“Akili zote” katika mstari huu ina maana fikra zote, na mawazo yote, na mitazamo yote, na uelewa wote, na ufahamu wote unaotokana na akili!
Hebu tuitizame kwa pamoja faida hii, kwa kuangalia mfano wa eneo lifuatalo:
“Kutafuta uongozi wa Mungu, juu ya jambo lolote”.
Mithali 23:4b inasema: “…acha kuzitegemea akili zako mwenyewe”. Na Mithali 3:5 inasema: “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe”.
Ingawa Biblia inaturuhusu, na kutuhimiza kuzitumia akili (Waebrania 5:14), lakini inatukataza tusizitegemee akili. Biblia inatuhimiza tuitumie “amani ya Mungu”, kuthibiti matumizi ya “akili zote” (Wafilipi 4:7).
Na kwa sababu hiyo, hutakiwi kuzitegemea akili (au fikra au mawazo), katika kutafuta uongozi wa Mungu, juu ya jambo lolote, bali tegemea amani ya Kristo, katika kuchagua ni fikra ipi ya kuifuata, au ni wazo lipi la kulifuata.
Hii ni kwa sababu, fikra na mawazo katika akili zako, si za kutegemewa kukuongoza, bila amani ya Mungu kuhusika!
Biblia inasema: Katika kila wazo, au fikra, au neno…“Utafute amani ukaifuate” (Zaburi 34:14). Na kwa sababu hiyo – “mtaongozwa na amani” (Isaya 55:12b).
Na ikiwa fikra, au wazo, vinakuongoza kwenye njia iliyopotoka, nje ya Mungu, utajikuta umekosa amani moyoni mwako!
Hii ni kwa sababu, wale wapitao katika njia iliyopotoka, hawana amani mioyoni mwao (Isaya 59:8). Tena “Wala njia ya amani hawakuijua” (Warumi 3:17).
Angalizo: Fikra yo yote moyoni mwako, isiyokubali kutawaliwa na kuongozwa na amani ya Kristo, usiifuate! Na usilifuate wazo lolote moyoni mwako, lisilokubali kutawaliwa, na kuongozwa na amani ya Kristo!
Kumbuka:
Jizoeze kuombea akili zako, na fikra zako, na mawazo yako, na mtazamo wako, vikubali kutawaliwa, na kufanya kazi chini ya amani ya Mungu, iliyo moyoni mwako kwa njia ya Yesu Kristo. Akili zako unapozitumia, zisipotoa ushirikiano kwa amani ya Mungu ndani yako, ni rahisi zikakupotosha na wakati huo huo usijue kama umepotoka!

The post Faida za kuombea akili, ili kuimarisha Imani yako, maisha yako-2 appeared first on Mana.

]]>
5177
Faida za kuombea akili, ili kuimarisha imani yako, na maisha yako-1 https://mwakasege.org/kuombea-akili/?utm_source=rss&utm_medium=rss&utm_campaign=kuombea-akili Thu, 05 May 2022 16:01:20 +0000 http://beta.unitedthemes.com/brooklyn/?p=4098 Bwana Yesu asifiwe Tunaamini unaendelea vizuri. Leo nataka nianze kukuletea mfululizo wa masomo, yanayohusu: “Faida za kuombea akili, ili kuimarisha imani yako, na maisha yako”. Ninapoziandika faida hizi, siziandiki kwa mtiririko wa umuhimu. Naziandika kwa mtiririko wa mfuatano wa kiuandishi tu, faida zote ni muhimu! Faida ya 1 ya kuombea akili: MUNGU AKUSAIDIE, KUJUA MATUMIZI […]

The post Faida za kuombea akili, ili kuimarisha imani yako, na maisha yako-1 appeared first on Mana.

]]>
Bwana Yesu asifiwe
Tunaamini unaendelea vizuri. Leo nataka nianze kukuletea mfululizo wa masomo, yanayohusu: “Faida za kuombea akili, ili kuimarisha imani yako, na maisha yako”. Ninapoziandika faida hizi, siziandiki kwa mtiririko wa umuhimu. Naziandika kwa mtiririko wa mfuatano wa kiuandishi tu, faida zote ni muhimu!

Faida ya 1 ya kuombea akili:

MUNGU AKUSAIDIE, KUJUA MATUMIZI YA AKILI ALIZOKUPA, ILI UWEZE KUZITUMIA IPASAVYO, KAMA ALIVYOKUSUDIA.
Mungu alipomuumba mtu, alimuumba awe jumlisho la roho, na nafsi, na mwili (2 Wakorintho 7:1). Mtu ni roho, anayo nafsi, na anakaa ndani ya mwili!
Mtu aliumbwa aweze kuishi, kwenye ulimwengu mbili kwa wakati mmoja – yaani ulimwengu wa kiroho, na ulimwengu wa kimwili kwa pamoja, na kwa wakati mmoja.
Mtu aliumbwa awe roho, ili kwa njia ya roho, aweze kuishi katika ulimwengu wa roho (Mwanzo 1:26, 27). Na kwa mwili wake, aweze kuishi katika ulimwengu wa kimwili (Mwanzo 2:7).
Na mtu alipewa nafsi, ili iwe “kiungo”, kati ya roho na mwili. Na kwa ajili ya jukumu hilo, nafsi ni kiungo muhimu cha mtu, katika kuunganisha maisha yake ya kiroho, na ya kimwili.
Ndiyo maana roho ya mtu, ndiyo iliyoumbwa kwanza (Mwanzo 1:27). Mwili wa mtu, uliumbwa wa pili (Mwanzo 2:7a). Na nafsi ya iliumbwa ya tatu (Mwanzo 2:7b)
Biblia inasema: “Bwana Mungu…, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai” (Mwanzo 2:7). Na ukisoma Ayubu 32:8; utasoma maneno haya: “Lakini imo roho ndani ya mwanadamu, na pumzi za Mwenyezi huwapa akili”.
Mistari hiyo miwili, inatupa kujua, na kuamini kuwa, akili imo ndani ya Nafsi!
Lakini pia, ni vizuri ujue ya kuwa, akili siyo ubongo, na ubongo siyo akili; ingawa vyote viwili viliumbwa ili vifanye kazi kwa kushirikiana! Ubongo umo katika mwili, na akili imo katika nafsi!
Biblia inatuelekeza tusizitegemee akili! Imeandikwa katika Mithali 3:5, 6; kuwa: “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako”.
Na Mithali 23:4 inasema: “…acha kuzitegemea akili zako mwenyewe”.
Pamoja na maagizo ya biblia, kwamba tusizitegemee akili, inatuhimiza pia, kuwa tuzitumie akili! Hii inatujulisha kuwa, Mungu aliziumba akili ndani ya kila mtu, ili azitumie, lakini asizitegemee!
Biblia inasema: “…Kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya” (Waebrania 5:13, 14).
Faida mojawapo ya kuombea akili, ni ili Mungu akusaidie kujua matumizi ya akili alizokupa, ili uweze kuzitumia hizo akili, kama alivyokusudia!
Tena, kumbuka, bila msaada wa Mungu, si rahisi sana ukaweza kuzitumia akili bila kuzitegemea! Lakini Mungu, anao uwezo wa kukusaidia, uweze kuzitumia akili, na usizitegemee, bali umtegemee Yeye!
Ombea akili ili ujue matumizi yake! Kitu usichojua matumizi yake, ni rahisi kukitumia vibaya; au hutakitumia kwa kiwango kinachotakiwa! Na kitu ulichonacho, na huijui faida yake kwako, si rahisi pia kukikumbuka kukiombea ipasavyo! Zijue faida za akili, ili uweze kukumbuka kuziombea mara kwa mara!
Tuzidi kuombeana katika hili!

The post Faida za kuombea akili, ili kuimarisha imani yako, na maisha yako-1 appeared first on Mana.

]]>
4098